Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umasikini umekuwa ada kwa wafanyakazi duniani: ILO

Mfanyakazi wa Vita Foam anafanya kazi kwa bidiii huko Freetown, Sierra Leone (Maktaba Juni 2015)
Dominic Chavez/Benki ya Dunia
Mfanyakazi wa Vita Foam anafanya kazi kwa bidiii huko Freetown, Sierra Leone (Maktaba Juni 2015)

Umasikini umekuwa ada kwa wafanyakazi duniani: ILO

Ukuaji wa Kiuchumi

Mamilioni ya watu kote duniani wanafanya kazi, lakini bado wanaishi kwenye umasikini mkubwa. 

Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya karibuni ya shirika la kazi duniani ILO ikionyesha kwamba hatua zaidi zinahitajika ili kupunguza pengo la kutokuwepo usawa na kuboresha mazingita ya wafanyakazi masikini ambao wanakabiliwa hali mbaya kila uchao.

Akizungumzia hali hiyo Stefan Kühn, mwandishi mkuu wa ripoti hiyo “Mtazamo wa ajira kwa mwaka 2018 au WESO Trends 2018” amesema ajira dunia zinaathiri wafanyakazi 3 kati ya 4 katika nchi zinazoendelea huku mwaka 2017 ilikadiriwa kuwa wafanyakazi milioni 1.4 walikuwa katika ajira duni na wengine milioni 17 wakitarajiwa kujiunga nao mwaka huu.

Ametoa mfano wa Bi Louisette Fanjamalala aliyefanya kazi kwa bidii miaka mingi kwenye kiwanda cha nguo mjini Malagasy Madagascar lakini hadi ameshindwa kuhifadhi hata senti Benki akiishi na watoto wanne katika hali ya umasikini , na kibaya zaidi sasa anakabiliwa na changamoto nyingine

(SAUTI YA LOUISETTE FANJAMALALA)

Kwa mujibu wa ILO hali kama hiyo inawakabili mamilioni ya wafanyakazi wengine sehemu mbalimbali duniani na hasa nchi zinazoendelea.