Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Martin Kobler awaomba wabunge wa Libya kuelewana kuhusu serikali

Martin Kobler awaomba wabunge wa Libya kuelewana kuhusu serikali

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu nchini Libya, Martin Kobler, amelaani kukwama kwa mchakato wa amani nchini Syria, akiwaomba wabunge kuikubali serikali jumuishi iliyopendekezwa kuundwa kupitia makubaliano ya amani.

Ameeleza hisia zake leo wakati akihutubia kikao cha Baraza la Usalama mjini New York Marekani, akiongeza kwamba ukosefu wa utawala wa sheria unasababisha vikundi vya kigaidi na uhalifu kustawi nchini humo.

Bwana Kobler amesisitiza kwamba iwapo serikali jumuishi haitaapishwa, nchi itakuwa hatarini kufilisika na kusambaratika.

Mapendekezo ya serikali mpya yamepelekwa bungeni mwezi Januari mwaka huu na kukatiliwa, mapendekezo mengine yakipelekwa tena mwezi Februari lakini Bunge limekata kuyaridhia licha ya idadi kubwa ya wabunge kuyakubali, ameeleza Bwana Kobler akiwasihi wawakilishi hao kusonga mbele katika mchakato wa amani na kuapisha serikali mpya.