Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashauriano ya dhati ndio njia pekee ya amani Mashariki ya Kati: Serry

Mashauriano ya dhati ndio njia pekee ya amani Mashariki ya Kati: Serry

Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kwenye mchakato wa amani huko Mashariki ya Kati, Robert Serry amesema mwendelezo wa mapigano ya kusikitisha kwenye eneo hilo inadhahirisha vile mamlaka zilizoko zisivyo na mashiko.

Akitoa taarifa yake mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo mjini New York, Marekani kuhusu hali ya usalama Mashariki ya Kati, Serry amesema hakutakuwepo na maendeleo yoyote iwapo uhalali wa hofu ya Israeli juu ya usalama wake hautashughulikiwa, jambo ambalo amesema wakati huo huo litatoa fursa ya utulivu kama itawezesha kuondolewa kwa vizuizi huko Gaza.

(SAUTI YA SERRY)

Wiki iliyopita kutokana na hali iliyokuwepo Gaza ilikuwa nusura tuingie kwenye mgogoro ambao ungesambaa eneo lote. Tunapaswa kuchukulia hali ile kama onyo kwetu sote kushirikiana kurejesha matumaini ya amani. Hatma ya eneo hilo imegubikwa na giza. Hata hivyo kinachofahamika ni kwamba mgogoro kati ya waarabu na waisraeli hauwezi kupuuzwa kwani unatoa mwelekeo wa baadaye wa eneo hilo. Bado nina imani kuwa suluhu ya mzozo kati ya Israeli na Palestina ni mashauriano ya dhati ya kuwa na mataifa mawili na hili litaleta utulivu kwenye eneo hilo.”