Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yatangaza kutokea kipindi cha El Nino

WHO yatangaza kutokea kipindi cha El Nino

Shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WHO linasema huenda kukawa na kipindi kilicho dhaifu cha El Nino mwezi Septemba na Oktoba na kuendelea hadi kutakapoanza msimu wa baridi kaskazini mwa dunia. Kipindi cha El Nino kina dalili za joto juu ya bahari katikati na mashariki mwa bahari ya Pacific kinyume na hali ya baridi juu ya bahari wakati wa kipindi cha La Nina. Vipindi vya El Nino na La Nina vina athari kwa hali ya hewa na mazingira kote duniani.

Katibu mkuu wa WMO Michel Jarraud amesema uwezo wa shirika hilo la kutabiri siku za usoni umeimarika hasa utabiri wa vipindi vya El Nino na La Nina hatua ambayo imechangia katika kupunguza hatari za majanga ya kiasili. WHO kwa sasa inaongoza jitihada za kimataifa za kuboresha huduma za utabiri wa hali ya hewa kupitia utabiri wa kila mara. Mwishoni mwa mwezi Oktoba kutaandaliwa mkutano kuhusu utabiri wa hali ya hewa ambao utatekeleza mpango kuhusu huduma za utabithi wa hali ya hewa duniani.