Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ugonjwa wa Novel Coronavirus waripotiwa Uingereza

Ugonjwa wa Novel Coronavirus waripotiwa Uingereza

Taifa la uingereza limelifahamisha shirika la afya duniani WHO kuhusu ugonjwa wa Novel Corovirus ambayo ni homa hatari inayofananishwa na homa ya mafua ya Sars iliyo na historia ya kuambukiza kupitia usafiri kwenda nchini Saudi Arabia na Qatar. Mwanamme wa umri wa miaka 49 raia wa Qatar alionekana akiwa na dalili za ugonjwa huo tarehe 3 mwezi Septemba mwaka huu na anaripotiwa kusafiri wakati mmoja kwenda nchini Saudi Arabia.

Tarehe saba mwezi huu mwanamme huyo alilazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi mjini Doha, Qatar na kusafirishwa baadaye tarehe 11 hadi nchini Uingereza ambapo alifanyiwa utafiti wa mahabara na kubainika kuwa anaugua ugonjwa huo. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)