Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kongamano la IAEA lalenga matumizi ya nguvu za nyuklia katika uzalishaji wa kilimo

Kongamano la IAEA lalenga matumizi ya nguvu za nyuklia katika uzalishaji wa kilimo

Kongamano la kutumia sayansi ya nyuklia kwa njia ya amani katika masuala ya kilimo, linaendelea mjini Vienna, Austria.

Kongamano hilo ambalo limeandaliwa na Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki, IAEA, linaleta pamoja wawakilishi kutoka nchi zinazokubali mwelekeo wa IAEA, wa kutumia teknolojia ya sayansi ya nyuklia kwa njia ya amani.

Ili kufahamu zaidi, nimezungumza na Profesa Miriam Kinyua, ambaye ni mhadhiri wa Bayoteknolojia kutoka Chuo Kikuu cha Moi nchini Kenya anayehusika na utafiti katika mimea ya ngano na mihogo, na ambaye amealikwa kwenye kongamano hilo ili kuzungumzia teknolojia ya nyuklia inayoweza kutumiwa kwa uzalishaji wa chakula cha kutosha kwa siku zijazo.

(SAUTI YA MIRIAM KINYUA)