Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Yemen imeanza kuimarika kidemokrasia:UM

Yemen imeanza kuimarika kidemokrasia:UM

Yemeni ambayo hivi karibuni ilitumbukia kwenye mkwamo wa kisiasa, imeanza kupiga hatua kusonga mbele licha kwamba inakabiliwa na vizingiti vya hapa na pale.

Hayo ni kwa mujibu wa mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa ambaye amesisitiza haja ya kuendelea na jitihada za kulifanyia mageuzi jeshi la taifa hilo.

Taifa hilo linapitia kwenye vugu vugu la mabadiliko ya kidemokrasia baada ya rais wa wakati huo kuondoka madarakani na kumpisha msaidizi wake Abdrabuh Mansour Hadi Mansour,.

Kwa mujibu wa mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa Jamal Benomar, taifa hilo sasa linapiga hatua kusonga mbele na ameelezea kuridhishwa kwake na mifumo ya kiutawala inavyofanya kazi.