Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Teknolojia ya Nyuklia inasaidia upatikanaji wa chakula hapo baadaye:IAEA

Teknolojia ya Nyuklia inasaidia upatikanaji wa chakula hapo baadaye:IAEA

Kwa takribani miaka 50 matumizi ya teknolojia ya nyuklia yamekwa yakisaidia wakulima duniani, kuchangia katika mazao mbalimbali, kudhibiti wadudu, uchunguza maradhi ya mifugo, kuboresha udongo na kudhibiti maji na kuongeza usalama wa chakula.

Na umuhimu wa teknolojia ya nyuklia katika kusaidia kilimo itakwa ndio ajenda kuu kwenye kongamano la kisayansi la mwaka huu la shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA litaklalofanyika Vienna Austria kuanzia Septemba 18 hadi 19. Kauli mbiu ya kongamani ni “chakula kwa ajili ya baadaye:kukabili changamoto kwa kutumia nyuklia.

IAEA inashirikiana na shirika la chakuula na kilimo FAO katika kutoa msaada kuupitia kitengo chake cha Vienna. Kongamano hilo litafunguliwa na mkurugenzi mkuu wa FAO Graziano da Silva na litajadili shughuli za IAEA katika uupande wa uzalishaji, ulinzi na usalama wa chakula.Yukiya Amano ni mkurugenzi mkuu wa IAEA

(SAUTI YA YUKIYA AMANO)