Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Michuano ya Olympic London imevuka viwango:UM

Michuano ya Olympic London imevuka viwango:UM

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa unazingatia amani ndani ya michezo umepongeza mafanikio yaliyopatikana katika michezo ya Olimpiki iliyomalizika hivi karibuni ni ile maalumu kwa ajili ya watu wenye ulemavu Paralympic.

Ujumbe huo umesema kuwa mashindano ya mwaka huu 2012 Jijini London yameweka rekodi ya kuvutia na kuacha ujumbe unaotia matumaini kwa kila mmoja.

 Katika taarifa yake mkuu wa ujumbe huo Wilfried Lemke,amesema kuwa serikali ya Uingereza kwa kushirikiana na kamati ya kimataifa ya Olimpiki wamefaulu kuvuka malengo.