Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ugonjwa wa Kipindupindu waendelea kusambaa nchini Sierra Leone

Ugonjwa wa Kipindupindu waendelea kusambaa nchini Sierra Leone

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa mkurupuko wa ugonjwa wa kipindupindu nchini Sierra Leone hauna dalili zozote za kudhibitika. Hadi mwishoni mwa juma lililopita visa 16,360 viliripotiwa huku watu 250 wakiaga dunia. Kulingana na WHO mji mkuu wa Freetown unaripoti visa vingi zaidi huku asilimia 60 ya visa vipya vikiripotiwa kwenye mji huo.

 WHO inashirikiana kwa karibu na serikali ya Sierra Leone kuudhibiti ugonjwa huo baada ya rais wa nchi hiyo kuutangaza ugonjwa wa kipindupindu kuwa janga la kibinadamu. Awali kulibuniwa jopo kazi la rais ambalo limetwikwa juku la kuratibu na kutafuta mbinu ya kuudhiti ugonjwa huo. Kupitia msaada wa mashirika kadha ya kimataifa wizara ya afya inaongoza jitihada za kuukabili ugonjwa huo