Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya watu wanaonyongwa yazidi kuongezeka:UM

Idadi ya watu wanaonyongwa yazidi kuongezeka:UM

Umoja wa Mataifa umeelezea wasi wasi wake kutokana na kuendelea kuongezeka kwa idadi ya watu wanaonyongwa kutoka na uhalifu tofauti nchini Gambia, Sudan Kusini na Iraq. Hivi majuzi watu 6 walinyongwa nchini Gambia hata baada ya kutishwa kwa sheria hiyo tangu mwaka 1985. Nchini Iraq watu 26 wamenyongwa mwezi huu.

UM unasema kuwa kesi zinazosababishwa watu hao kunyongwa sio wazi. Nchini Sudan kusini wanaume wawili walinyongwa siku ya Jumanne ambapo ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa inasema kuwa wawili hao hawakupewa huduma za kisheria za kujitetea zilizohitajika. Ofisi hiyo inatoa wito kwa mataifa kuondoa sheria ya kunyonga huku mataifa 150 hadi sasa yaliwa yamepiga marufuku sheria ya hukumu ya kifo. Chini ya sheria ya kimataifa hukumu ya kifo inaweza kutumika kwenye kesi zenye uzito hasa mauaji.