Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua zimepigwa lakini bado kuna changamoto ya watu kutoweka Chile:UM

Hatua zimepigwa lakini bado kuna changamoto ya watu kutoweka Chile:UM

Uchunguzi na kuchukuliwa kwa hatua dhidi ya watu kutoweka kwa lazima ni mafanaikio muhimu kwa serikali ya Chile na jamii katika vita dhidi ya ukwepaji sheria kwa kukiuka haki za binadamu.

Hayo yamesema na wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanaohusika na watu kutoweka bila hiyari yao waliohitimisha ziara yao nchini Chile.

Wameongeza kuwa pamoja na hatua hizo zilizopigwa bado kuna changamoto nyingi zilizosalia. Wamesema ni watuhumumiwa wachache saana waliohukumiwa kwa kuhusika na utowekaji wa watu ambao wanatumikia kifungo kutokana na faini ndogo walizopewa au msamaha waliopewa. Alice Kariuki anaripoti

(TAARIFA YA ALICE KARIUKI)