Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama laongeza muda wa UNAMID kwa kipindi cha mwaka mmoja

Baraza la Usalama laongeza muda wa UNAMID kwa kipindi cha mwaka mmoja

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limeongeza muda wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika jimbo la Darfur, UNAMID kwa kipindi cha mwaka mmoja.

UNAMID, ambayo inajumuisha vikosi vya Umoja wa Mataifa na vile vya Muungano wa Afrika, iliundwa mwaka 2007 ili kuwalinda raia ambao walilazimika kuhama makwao kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2003 katika jimbo la Darfur, magharibi mwa Sudan, na kusaidia kutafuta suluhu ya kisiasa kwa mzozo huo.

Mataifa 14 wanachama wameunga mkono azimio nambari 2063, la kuongezwa kwa muda wa UNAMID, isipokuwa Azerbaijan, ambayo haikuegemea upande wowote.

Balozi wa Uingereza kwenye Umoja wa Mataifa, Mark Grant amewaelezea waandishi wa habari zaidi kuhusu azimio hilo