Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Timor-Leste imepiga hatua za amani na salama lakini umasikini bado upo:UM

Timor-Leste imepiga hatua za amani na salama lakini umasikini bado upo:UM

Timor Leste imepgia hatua muhimu katika kuimarisha amani na usalama, na kushuhudia maendeleo ya kiuchumi kwa kasi, Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu umaskini wa kupindukia na haki za binadamu Bi. Magdalena Sepulveda Carmona ameliambia Baraza la Haki za Binadamu, mjini Geneva.

Licha ya hatua hizo, bado kuna hali ya umaskini uliokithiri na ongezeko la mwanya wa kiuchumi ambao umejisitiri kwenye vigezo vya ukuaji wa kiuchumi. Ukuaji wa kiuchumi wa hivi karibuni haujachangia kubadilika kwa halia ya maisha ya watu kwa njia endelevu, au kufungua nafasi za ajira kwa idadi kubwa ya raia wa Timor Leste.

Umaskini bado ni mkubwa, na umesambaa, kwani asilimia 41% ya idadi ya watu wa Timor Leste wanaishi kwa chini ya dola moja kwa siku. 58% ya watoto wana lishe duni, na ukosefu wa ajira au hatari ya kupoteza ajira inakadiriwa kuwa 70%.