Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MINUSTAH yashirikiana na polisi kukabili silaha haramu Haiti

MINUSTAH yashirikiana na polisi kukabili silaha haramu Haiti

Umoja wa Mataifa unaisaidia serikali ya Haiti katika kupambana na silaha haramu. Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MINUSTAH na jeshi la taifa la polisi wiki hii wameanza operesheni ya pamoja ya kushika doria nchini Haiti katika vitongoji mbalimbali kwenye mji mkuu Port-au-Prince ili kuzuia usambazaji wa silaha.

Kwa mujibu wa MINUSTAH kuna ongezeko la idadi ya silaha haramu nchini humo yakiwemo makundi ya watu wenye silaha wanaodai kuwa ni sehemu ya jeshi, ambalo bado halijaanzishwa na serikali.

Jim Hoeft msemaji wa MINUSTAH amesema lengo lao ni kuisaidia serikali ya Haiti kuanzisha utawala wa sheria na kuweka mazingira mazuri kwa watu wa nchi hiyo ili waweze kujihusisha na biashara na hatimaye kUishi kwa amani.