Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake wakimbizi bado wanaendelea kuathirika nchini Haiti

Wanawake wakimbizi bado wanaendelea kuathirika nchini Haiti

Punde tu baada ya tetemeko kubwa la ardhi kuikumba Haiti takriban watu milioni 1.5 walijipata wamedugwaa kwenye barabara zilizojaa vifusi baada ya karibu nyumba 80,000 kuporomoka. Miaka miwili tangu kulipotokea tetemeko bado zaidi ya watu 650,000 wanaishi kwenye kambi kwenye mazingira mabaya. Hata baada ya kuchaguliwa rais mpya nchini Haiti mwezi Mei mwaka uliopita bado serikali ya Haiti inakabiliwa na changamoto nyingi.

Mashirika mengi yasiyokuwa ya kiserikali na ya Umoja wa Mataifa yanajiandaa kusitisha oparesheni za gharura hatua ambayo hata hivyo inaonekana kuwa changamoto kubwa kwa kuwa bado watu wengi wako kambini. Kati ya wasio na makao wanawake ndio huathirika zaidi hasa kupitia kwa dhuluma za kingono.