Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usalama wa chakula ni suala la kulipa kipaumbele Haiti:WFP

Usalama wa chakula ni suala la kulipa kipaumbele Haiti:WFP

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasema pamoja na hatua zilizofikiwa miaka miwili baada ya tetemeko nchini Haiti suala la usalama wa chakula bado linahitaji kupewa kipaumbele.

Hata hivyo shirika hilo linasema kuwa ushirikiano na serikali ya Haiti na wadau wengine yakiwemo mashirika ya Umoja wa Mataifa wamepiga hatua kubwa ya kuimarisha usalama wa chakula na WFP inaendelea kutoa msaada wa chakula kwa watu milioni 1.5 kisiwani humo. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)