Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ataka pande zinazozozana nchini Iraq kuketi meza moja

Ban ataka pande zinazozozana nchini Iraq kuketi meza moja

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea shaka yake juu ya kuendelea kwa mkwamo wa kisiasa nchini Iraq na amezitaka pande zote kuketi meza moja ya kutanzua hali hiyo katika hali ya amani na usalama.

Katika taarifa yake iliyotolewa kupitia msemaji wake, Ban amesema kuwa anaitizama hali ya kisiasa ya Iraq kwa sura ya wasiwasi na kuongeza kuwa iwapo hali hiyo itaachwa iendelee inaweza kusababisha uhalibifu mkubwa wa amani na usalama.

Ametaka pande zote kuweka shabaya ya pamoja ili kutafutia suluhu mikwamo midogo midogo ya kisiasa iliyosalia na wala siyo kufanya vinginevyo.

Ban ameongeza kusema kuwa katika wakati serikali ya Iraq ikikaribisha mwaka mpya mnamo wakati vikosi vya kigeni vikijindoa kabisa kwenye ardhi ya nchi hiyo ni fursa tosha ya kuanzisha mshikamano mpya na mwendeleza maridhawa wa taifa hilo katika ujenzi wa demokrasia imara.