Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yatangaza mpango wa kukarabati majengo ya Pompeii

UNESCO yatangaza mpango wa kukarabati majengo ya Pompeii

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa imekubaliana kufanya kazi na serikali ya Italy ili kulinusuru eneo la Pompeii ambalo kwa sasa lipo kwenye hali mbaya. Pompeii ambayo inakusanya kumbukumbu za kiujenzi wa kale ni moja ya eneo hadimu linalohifadhi uruthi wa dunia.

Shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia masuala ya elimu sayansi na utamaduni UNESCO limesema kuwa linatazamia kukamilisha ukarabati wa jingo hilo katika kipindi cha miezi nane ijayo. Jengo hilo lilipoteza sura yake baada ya kuharibiwa na mvua kubwa mapema mwaka jana. Maeneo kadhaa ikiwemo pia nyumba ya kifamle ilibomoka kutokana na mvua hiyo.