Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa UM kuchunguza visa vya kutoweka kwa watu

Wataalamu wa UM kuchunguza visa vya kutoweka kwa watu

Wataalamu wa haki za binadamu kutoka Umoja wa Mataifa wanaohusika na masuala ya kutoweka kwa watu wameanza kufanyia ukaguzi kesi 400 zikiwemo za hivi majuzi. Kundi hilo la wataalamu watano kutoka UM litafanya mikutano na wajumbe wa serikali pamoja na mashirika ya umma mjini Geneva na familia za waliotoweka.

Kundi hilo pia litachunguza madai kuhusu vizingiti vilivyopo katika utekelezaji wa mkataba wa kulinda watu walioathiriwa na kutoweka kwa lazima.