Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lautaka utawala wa Libya kufifisha masalia ya silaha

Baraza la Usalama lautaka utawala wa Libya kufifisha masalia ya silaha

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeitaka mamlaka ya mpito ya Libya kuchukua hatua za haraka kudhibiti mtawanyiko wa silaha likionya kuwa iwapo hatua hiyo haitatekelezwa eneo hilo linaweza kuandamwa na hali mbaya ya usalama.

Nchi zote wanachama wa baraza hilo limeunga mkono azimio linalotaka mamlaka za Libya kuchukua hatua za makusidi kuharibu ama kuchoma moto masalia ya silaha zilizotumika wakati wa mapigano ya kuondoa utawala wa kanali Muamar Gaddafi.

Zingatio hilo limekuja katika wakati ambapo muda wa utawala wa mpito wa Libya ukifika ukingoni.