Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yatoa ripoti kuhusu hali ya uhamiaji barani Ulaya

IOM yatoa ripoti kuhusu hali ya uhamiaji barani Ulaya

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM leo limezindua ripoti inayozingatia hali ya uhamiaji na hali mbaya ya uchumi kwa nchi wanachama wa jumuiya ya muungano wa Ulaya.

Tatizo la uhamiaji katika nchi za muungano wa Ulaya ni kubwa, huku wahamiaji wengi wakikabiliwa na matatizo kadha wa kadha wanapoingia katika baadhi ya nchi hizo, kama kunyimwa haki na vibali vya kuishi, kufanya kazi na hata kupata huduma za afya.

Wengi wa wahamiaji hao ni kutoka katika nchi masikini zikiwemo za Afrika zilizoko kusni mwa Jangwa la Sahara. George Njogopa na ripoti kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Ripoti hiyo yenye kichwa cha habari kisemacho " Uhamiaji na mkwamo wa kiuchumi kwa nchi za Ulaya, imetokewa baada ya kufanyika utafiti katika nchi 27 wanachama wa Jumuiya hiyo na kubainisha kuwa, athari mbaya za uchumi zimehusika pakubwa kwenye uhamiaji.

Kulingana na ripoti hiyo, umekwamo wa uchumi uliokumba dunia hivi karibuni, umeleta mpangalanyiko kwenye uhamiaji , ingawa madhara yake yanaweza kudhihirika kuanzia kipinda cha mwaka mmoja toka sasa. Hata hivyo ripoti hiyo imesisitiza kuwa kiwango cha uhamiaji miongoni mwa nchi wanachama wa jumuiya hiyo kimepungua sana kwa sasa tangu kumalizika kwa kipindi cha mtikisiko wa uchumi.