Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO inazindua kampeni kubwa ya chanjo katika mabara matatu

WHO inazindua kampeni kubwa ya chanjo katika mabara matatu

Shirika la afya duniani WHO kwa mara ya kwanza kesho Aprili 24 litazindua kampeni ya chanjo kwa nchi 112. Kampeni hiyo itazigusa nchi za Marekani, Mediteranian Mashariki na Ulaya.

Lengo la kampeni ya chanjo hiyo ni kupanua wigo na kuelimisha umma umuhimu wa chanjo.

Kampeni hiyo italenga zaidi chanjo za magonjwa ya utotoni ambayo ynaweza kuzuilika kama surua, pepopunda na polio.