Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

KM wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon aliwasili Afrika Kusini siku ya Jumanne kuanza ziara yake ya nchi tano za Afrika, itakayomfikisha Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda na Misri.

Masuala muhimi yatakayo jadiliwa wakati wa ziara yake yatakua juu ya amani na usalama, mabadiliko ya hali ya hewa na utawala bora, pamoja na mkutano wa kuikarabati Gaza huko Misri, kituo cha mwisho cha ziara yake.

KM amepongeza siku ya Ijumanne, ahadi ya kuachiliwa huru wafungwa wa kisiasa iliyofikiwa kati ya serekali ya Sudan na kundi kuu la waasi wa Darfur. Ahadi ni sehemu ya makubaliano ya nia njema na hatua za kujenga imani ili kuweza kutanzua mzozo wa Darfur yaliyotiwa sahihi huko Doha Qatar, Febuary 17, kati ya serekali na kundi la JEM. KM alizihimiza pande zote pia kufanya kazi na mpatanishi mkuu wa kikosi cha pamoja cha Umoja wa Afrika na UM pamoja na serekali ya Qatar katika kukomesha uhasama na makubaliano mapana ya amani.

Wakati idadi ya wanaombukizwa na kipindupindu huko Zimbabwe imeongezeka kufikia elfu 83 na zaidi ya vifo elfu 3 mia nane, Naibu Mratibu wa huduma za dharura amewasili Harare. Bi Catherine Bragg ambae pia ni naibu KM kwa ajili ya huduma za kiutu yuko nchini humo kutathmini jinsi janga la kipindupindu linavyokabiliwa pamoja na mahitaji ya chakula. Ziara hiyo yake inafanyika wakati kunaripoti kwamba ugonjwa huo umesamba katika nchi jirani. Msemaji wa shirika la Afya Duniani WHO anasema Afrika Kusini imeripoti watu elfu kumi wameambukizwa na 54 wamefariki. Maelfu ya watu wanaripotiwa pia kuambukizwa huko Msumbiji, Zambia na Malawi.

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la UM , UNHCR lilieleza Jumanne kua inazidi kua na wasi wasi mkubwa kutokana na kuongezeka kwa mashmabulio dhidi ya raia huko mashariki ya Kongo katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, yanayofanywa na waasi wa kihutu kutoka Rwanda. Mashambulio hayo yamesababisha wakazi wengi kukimbia makazi yao, baada ya mji ya Kipopo, Remeka na Kamuobe kushambuliwa na wanamgambo wa kundi la FDLR