Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Olusegun Obasanjo, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Maziwa Makuu amearifu kwamba mamzungumzo ya upatanishi yanatarajiwa kuanzsihwa tena katika siku za karibuni baina ya Serikali ya JKK na wafuasi wa jeshi la mgambo la CNDP.

     George Charpentier, Mratibu wa Misaada ya Dharura katika Cote d'Ivoire ameongoza timu maalumu ya mashirika ya UM yenye kuhudumia misaada ya kiutu kutathminia hali katika sehemu ya magharibi ya nchi, na walijumuisha mashirika yasio ya kiserikali kwenye ziara hiyo. Charpentier na kundi lake walikutana na watawala wenyeji pamoja na wanakijiji waliong'olewa makazi waliorudi makwao katika mazingira magumu yaliokosa chakula, maji salama, na miundombinu ya afya. Takwimu za UM zimeonyesha kuanzia Septemba 2008 watu 70,000 waliong'olewa makazi walirejea makwao.

    Ameerah Haq, Mratibu wa UM kwa Sudan ametoa mwito unaotaka wahudumia misaada ya kiutu wa kimataifa waruhusiwe haraka kuwafikia raia muhitaji 100,000 ziada wa eneo la Muhajariya na kuwafadhilia huduma za kunusuru maisha, wao pamoja na raia waliopokwenye sehemu mbili nyengine katika Darfur Kusini. Kwa mujibu wa Haq mashirika ya kimataifa yanayohudumia kisaada ya kihali yamelaumu kwamba tangu tarehe 07 Februari yalijaribu kupata kibali cha kuruhusu ndege zao kwenda katika  maeneo husika, lakini walishindwa kupokea idhini hiyo kutoka wenye madaraka. Haq alihadharisha bilaya kibali kutolewa, halan, hali ya mamia elfu ya raia itaharibika haraka.

    Baraza la Usalama asubihi lilikutana kuzingatia riipoti mpya kuhusu shughuli za Kamati ya Vikwazo inayohusika na azimio 1718 juu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Umma wa Korea (Korea Kaskazini), kamati ambayo inaoongozwa na Balozi Baki Ilcin wa Uturuki. Kufuatia mashhaurianno hayo Baraza lilisikiliza uchanganuzi wa maofisa wa UM wanaoshughulikia maendeleo ya karibuni katika Usomali na mchango wa vikosi vya ulinzi amani vya Umoja wa Afrika viliopo huko. Taarifa hiyo ilitangazwa Ijumatano na Obasanjo kwenye mji wa Goma baada ya kumaliza mashauriano na wawakilishiwa makundi husika. Alibainisha kwamba wahusika wote hawo wangelipendelea mazungumzo yao yafanyike nchini mwao. Obasanjo aliwasili JKK Ijumanne na alizuru yale maeneo yalioathirika na vurugu liliotukia huko katika wiki za karibuni.