Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lakutana tena kusailia mgogoro wa Ghaza

Baraza la Usalama lakutana tena kusailia mgogoro wa Ghaza

Baraza la Usalama limekutana Ijumatano magharibi, kwenye kikao cha dharura, kuzingatia mswada wa azimio liliodhaminiwa na Libya, kwa niaba ya Mataifa Wanachama wa Umoja wa Nchi Huru za KiArabu, kuhusu uwezekano wa kusimamisha mapigano yaliozuka katika eneo la WaFalastina liliokaliwa la Tarafa ya Ghaza. Kwenye risala mbele ya kikao hicho, KM Ban Ki-moon alikumbusha ya kuwa mtiririko wa mgogoro uliofumka Ghaza siku ya leo umeingia siku ya tano. Alisema raia wa KiFalastina, wanaojumuisha mfumo wa jamii hakika ya Tarafa ya Ghaza, pamoja na mpango wa amani kwa siku za

siku za usoni, ikichanganyika na utulivu wa kieneo na nia njema ya umma wa kimataifa – mambo yote haya sasa yamenaswa kwenye hali ya kutokuwa na dhamana, iliodhihirishwa na mashambulio yasiobagua ya makombora ya WaFalastina wafuasi wa kundi la Hamas [dhidi ya Israel], kwenye vitendo visowiana vilivyojionyesha dhahiri kutokana na hujuma kuu na mashambulio yanayoongozwa na majeshi ya Israel dhidi ya wakazi wa Ghaza. KM alihadharisha hali hii itaendelea kuhatarishwa amani ya eneo pindi mgogoro huu “utaselelea na kupanukia kiwango cha awamu ya vurugu liliojaa mauaji na maangamizi.” Aliendelea kueleza kwamba matokeo ya mgogoro uliojiri sasa katika Ghaza, wa vurugu na matumizi ya nguvu, umezusha hali ya kutisha sana kwa maisha ya WaFalastina milioni 1.5 wanaoishi katika maisha yaliopambwa na mashambulio mazito ya mabomu. Alishtumu na kulaani vikali, kwa msiamamo ulio wazi “mashambulizi ya makombora ya Kundi la Hamas na wapambanaji wengine wa KiFalastina.” Vile vile KM alisisitiza kuwa anashutumu “mashambulio yaliopita kiasi ya Israel” katika Ghaza. Aliyataka makundi yote husika na uhasama, kuhishimu na kutekeleza sheria za kiutu za kimataifa” kwa kuwapatia hifadhi raia, maana fungu hili la umma ndilo linaloathirika zaidi, na alipendekeza kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za haraka ili kukomesha usumbufu huu kwa jamii ya WaFalastina katika Ghaza.

Baraza la Usalama limemaliza kikao bila ya kupiga kura.