Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti ya UNMIL imeshtumu kutenguliwa haki za binadamu Liberia

Ripoti ya UNMIL imeshtumu kutenguliwa haki za binadamu Liberia

Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani Liberia (UNMIL) wiki hii limetangaza ripoti mpya kuhusu utekelezaji wa haki za binadamu nchini katika kipindi kilioanzia mwezi Mei hadi Oktoba mwaka jana. Ripoti ilisema kwamba ukaguzi wao ulifichua tabia ziliokwenda kinyume kisheria, mathalan, katika muda unaozingatiwa polisi wa taifa, pamoja na maofisa wa mahakama na maofisa wa magereza walikutikana kutengua haki za binadamu, kihorera, kwa kushiriki kwenye vitendo vya ulajirushwa. ~