Wapatanishi wa Kimataifa kwa Darfur wazuru Sudan kufufua mazungumzo ya amani
Wajumbe Maalumu wa Kimataifa kwa Darfur, yaani Salim Ahmed Salim wa Umoja wa Afrika na Jan Eliasson wa Umoja wa Mataifa wiki hii wapo Sudan wakijaribu kufufua, kwa kasi mpya, mazungumzo ya amani ambayo hivi karibuni yalionekana kupwelewa.