Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guinea-Bissau inakabili tishio dhidi ya utulivu wa amani

Guinea-Bissau inakabili tishio dhidi ya utulivu wa amani

Ripoti ya karibuni ya Baraza la Usalama kuhusu hali katika Guinea-Bissau imeonya kwamba kuselelea kwa mgawanyiko wa chuki kati ya wadau wa kizalendo, ni tukio lenye kuashiria mzoroto kwenye taasisi mbili muhimu za Taifa, yaani mahakama na bunge, kwa kulingana na kanuni za katiba. KM Ban Ki-moon amewanasihi wale wote wanaohusika na shughuli za utawala kuhakikisha wanatumia taratibu za kikatiba kusuluhisha ugomvi kati yao.