Mshindi wa Nansen Afrika 2019 kutoka DRC asema alichokifanya kinamridhisha
Pakua
Mshindi wa tuzo ya wakimbizi ya Nansen kwa kanda ya Afrika kwa mwaka huu wa 2019 Evariste Mfaume, amesema hata siku akikata pumzi, kile ambacho ameweza kufanya kuleta utangamano kati ya wakimbizi na wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kitakuwa kimetosha. Tuzo hiyo ya Nansen hutolewa na shirika la kuhudumia wakimbizi duniani, UNHCR.
Audio Credit
Arnold Kayanda/ Assumpta Massoi
Audio Duration
2'5"