Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

08 MACHI 2024

08 MACHI 2024

Pakua

Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Flora Nducha anamulika siku ya wanawake duniani kuanzia habari ya kwanza hadi ya mwisho maudhui yakiwa Wekeza kwa wanawake - songesha maendeleo.

  1. Katika kusherehekea siku ya wanawake duniani kote Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewapongeza wanawake na wasichana kwa kupata mafanikio makubwa na kuondoa vikwazo, kuvunja fikra potofu na kuchochea maendeleo kuelekea dunia yenye haki na usawa zaidi.
  2. Nchini Afrika Kusini katika jimbo la Western Cape kufuatia mafunzo kuhusu unyanyasaji wa kijinsia yaliyotolewa na kikundi cha wanawake cha Ilitha Labantu kwa vituo kadhaa vya polisi, sasa kuna ushahidi wa wazi kwamba vituo vya polisi vimeweka mazingira rafiki ya kuwasikiliza wanawake walionyanyaswa kuliko ilivyokuwa hapo awali. Anold Kayanda ameufuatilia mradi huo.
  3. Makala inatupeleka Kigoma nchini Tanzania kumsikia shuhuda Hadija Alisido ambaye amenufaika na miradi ya FAO.
  4. Mashinani tunabisha hodi Mwanza nchini Tanzania kupata maoni kuhusu siku ya wanawake duniani. Karibu!
Audio Credit
FLORA NDUCHA
Audio Duration
11'38"