Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF Rwanda: Programu ya “Winsiga Ndumva” waleta zawadi ya sauti kwa watoto viziwi

UNICEF Rwanda: Programu ya “Winsiga Ndumva” waleta zawadi ya sauti kwa watoto viziwi

Pakua

Kupitia mradi wa "Winsiga Ndumva", maneno ya lugha ya Kinyarwanda yanayomaanisha "Usiniache nyuma, ninaweza kusikia”, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kushirikiana na wadau wake ikiwemo Wizara ya Afya nchini Rwanda limebadilisha maisha ya watoto wengi na vijana ambao walikuwa na changamoto ya masikio na kuongea kwakuwapatia vifaa maalumu vya kupachika masikioni ili kusaidia masikio kufanya kazi yake ipasavyo. 

Huyo ni Vuguzima Francine, ambaye awali hakujua kuwa mtoto wake kwa kiasi kikubwa ni kiziwi. Mama huyu anasema, “nilikuwa ninamuadhibu kila siku kwa sababu nilikuwa nikimuita haitiki. Nikimwambia aende mahali haiendi. Nilifikiri ni kiburi. Kumbe baadaye ikagundulika hasikii.”

UNICEF, kwa zaidi ya watoto na vijana wadogo zaidi ya 500 katika maeneo kadha ya nchini Rwanda imefanya jambo ambalo wazazi na watoto wenyewe wanaona kama miujiza. Manirakora Emmnuel mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika kituo cha viziwi cha Butare akiwa na sura ya furaha na tabasamu pana anasimulia maisha yalivyokuwa magumu kabla hajapata machine ya kusaidia usikivu.

“Nilipokuwa ninacheza mpira na watoto wenzangu, mtu akiniambia nielekeze mpira kwake, nilikuwa sisikii. Kwa hiyo kwa kutojua nilikuwa napiga mpira popote.” 

Pongezi pia ziende kwa Kitengo cha Manunuzi au Ugavi cha UNICEF kilitekeleza jukumu muhimu kuhakikisha wanavipata visaidizi hivi vya masikio kwa dola 118 kila kimoja ingawa bei yake kwa kawaida inafikia dola 2000 za kimarekani. 

Audio Credit
Evarist Mapesa
Audio Duration
1'40"
Photo Credit
UNICEF Rwanda