Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kaveh Zahedi wa FAO: Hatuwezi kuwa tu watazamaji wa mabadiliko ya tabianchi, kilimo kina jukumu

Kaveh Zahedi wa FAO: Hatuwezi kuwa tu watazamaji wa mabadiliko ya tabianchi, kilimo kina jukumu

Pakua

Kilimo kinaweza kuchukua jukumu kuu katika hatua dhidi ya tabianchi wakati huo huo kikihakikisha uhakika wa chakula duniani, ni maoni ya Mkurugenzi wa Ofisi ya Mabadiliko ya Tabianchi, Bayonuai na Mazingira katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) Kaveh Zahedi kufuatia hivi majuzi mwaka 2023 kuthibitishwa kuwa mwaka wa joto zaidi katika rekodi za dunia. 

“Kwa hivyo, rekodi hizi ni muhimu. Sasa tunahitajika kuchukua hatua sasa. Hatuwezi tu kuwa aina ya watazamaji tu wa mabadiliko ya tabianchi, na kilimo kina jukumu kuu la kutekeleza". 

Bwana Zahedi anaongeza kusema kwamba kilimo endelevu kinaweza kuchangia katika kufikia uzalishaji sifuri wa hewa chafuzi.

“Mashamba hayapaswi tu kuwa wazalishaji wa chakula. Yanaweza kuwa vyanzo vya nishati mbadala. Nishati inaweza kutumika katika shamashamba ya ndani, kwa ajili ya kusukuma maji, kwa ajili ya umwagiliaji, au nishati ambayo inaweza kugawanywa katika gridi ya taifa, au taka za kilimo kugeuzwa kuwa nishati au nishati ya mimea. Hizi zote ni suluhisho za kilimo bora kwa nishati, na hiyo ndiyo aina ya kazi ambayo sisi FAO tumekuwa tukifanya na nchi." 

Audio Credit
Evarist Mapesa
Sauti
1'18"
Photo Credit
© FAO/Luis Tato