Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Madarasa yajengwa Sofala, Msumbiji kuhimili majanga ya asili ikiwemo vimbunga

Madarasa yajengwa Sofala, Msumbiji kuhimili majanga ya asili ikiwemo vimbunga

Pakua

Hii leo Umoja wa Mataifa umetoa ripoti ya kwanza ya uchambuzi wa aina yake kuhusu matukio ya watoto kulazimika kukimbia makwao kutokana na majanga yasababishwayo na hali ya hewa ikisema zaidi ya watoto milioni 43 walijikuta wakimbizi wa ndani kwenye nchi 44 katika kipindi cha miaka sita iliyopita, ikitafsiri kuwa ni watoto 20,000 kila siku.

Makadirio ya ripoti hiyo ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, yanaonesha kuwa kufurika kwa mito pekee kutafurusha watoto milioni 96 katika miaka 30 ijayo.

Kwa kutambua hilo, mafuriko yaliyosababishwa na kimbunga Idai nchini Msumbiji mwaka 2019  tayari yamekuwa somo na hatua zimechukuliwa, hatua ambazo zinaweza kuwa somo pia kwa maeneo mengine. Je ni hatua zipi hizo? Ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii iliyofanikishwa na UNICEF.

Audio Credit
Leah Mushi/Assumpta Massoi
Audio Duration
4'41"
Photo Credit
© UNICEF/UNI404964/Zuniga