Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtoto kuzaliwa njiti humtia hatarini kukumbwa na kifo, hatua zichukuliwe- WHO

Mtoto kuzaliwa njiti humtia hatarini kukumbwa na kifo, hatua zichukuliwe- WHO

Pakua

Inakadiriwa watoto milioni 13.4 njiti (wanaozaliwa kabla ya wiki 37 za ujauzito) walizaliwa mwaka 2020 idadi hii ikiwa ni takriban mtoto 1 kati ya 10 na wengi wa watoto hao ni kutoka Ukanda wa jangwa la Sahara na Asia ya Kusini imesema ripoti iliyochapishwa leo kwenye jarida la masuala ya afya la Lancet. Leah Mushi na maelezo zaidi.

Ripoti hiyo inafuatia utafiti uliofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO kwakushirikiana na lile la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF pamoja na Chuo kikuu cha London kitivo cha usafi na dawa za kitropiki (London School of Hygiene and Tropical Medicine.)

Mkurugenzi wa WHO idara ya masuala ya watoto wachanga, watoto, afya za barubaru na wazee Dkt. Anshu Banerjee amesema kwa kuwa watoto kuzaliwa kabla ya muda ni sababu kubwa ya vifo vya watoto wachanga suala hili linapaswa kushughulikiwa kwa udharura.

“Idadi hii inaonesha uhitaji wa uwekezaji wa maana ili kuweza kusaidia familia na watoto wao pamoja na kuweka mkazo katika katika kuhakikisha kuna upatikanaji wa huduma bora za afya kabla na wakati wa ujauzito.”

Sababu za kujifungua mtoto njiti

Hatari za afya ya uzazi, kama vile mimba za utotoni, maambukizi, lishe duni, na hali ya kutokwa na damu wakati wa ujauzito ni sababu zinazo husishwa na mama mjamzito kujifungua mtoto njiti.

Upatikanaji wa huduma bora wakati wa ujauzito ni suala muhimu kwani linawezesha kufanya utambuzi na udhibiti wa matatizo wakati wa ujauzito, kuhakikisha kuna uhesabuji sahihi wa ujauzito kwakuazia wakati mimba upo ndogo kupitia uchunguzi wa kutumia ultrasound na pale inapohitajika kuchelewesha mwanamke kupata uchungu wa kujifungua itawezekana kupitia matibabu yaliyo idhinishwa

Athari za kuzaliwa njiti

Taarifa ya WHO iliyotolewa leo kutoka huko Jijini Geneva Uswisi imebainisha kuwa mbali na suala la watoto kupoteza maisha, watoto njiti wanakabiliwa na ukuwaji wenye changamoto ikiwemo kupata magonjwa makubwa, ulemavu na ukuaji kwa kuchelewa na hata wakiwa wakiwa watu wazima wanaweza kupata magonjwa sugu kama kisurari na magonjwa ya moto.

“Watoto njiti wapo hatarini sana kupata matatizo ya afya yanayo hatarisha maisha na wanahitaji uangalizi maalum” amesema Dr. Banerjee

Matokeo ya utafiti

Utafiti huo Makadirio ya kwenye karatasi, ya Kitaifa, kikanda na kimataifa ya watoto njiti kwa mwaka wa 2020, yenye muelekeo kuanzia mwaka 2010: uchambuzi wa kiutaratibu,umeonesha kuna utofauti baina ya kanda na mataifa.

Asilimia 65 ya watoto njiti waliozaliwa mwaka 2020 walitokea Kusini mwa jangwa la Sahara, na Asia Kusini watoto njiti walikuwa asilimia 13.

Nchi zilizoathiriwa zaidi ni Bangladesh 16.2%, Malawi 14.5% na Pakistan 14.3%.

Utafiti huo umeonesha suala la watoto njiti sio la nchi tajiri au masikini wajawazito wote wanaweza kuathirika katika kila kona ya dunia. Kuna takwimu zinazoonesha zaidi kuwepo kwa idadi kubwa ya watoto njiti katika nchi tajiri mfano 11.6% nchini Ugiriki na 10% nchini Marekani.

Audio Credit
Anold Kayanda/Leah Mushi
Audio Duration
3'5"
Photo Credit
Doris Mollel Foundation