Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukatili wa kingono katika mizozo ni jinamizi lililokita mizizi katika pengo la usawa: UN

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili wa kingono katika mizozo ya vita Umoja wa Mataifa umesenma jinamizi hilo ni janga lililokita mizizi katika kukosekana kwa usawa na kanuni na tamaduni kali za masuala ya kijinsia. Tupate maelezo Zaidi kutoka kwa Flora Nducha

(TAARIFA YA FLORA NDICHA)

Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa leo mjini Brussells na New York na mwakilishi wa pamoja wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili wa kingono katika mizozo Pramila Patten na mwakilishi wa Muungano wa Ulaya kwa ajili ya mambo yan je na sera za usalama Josep Borrell wametoa wito wa hatua madhubuti zaidi za kuzuia na kukomesha unyanyasaji wa kingono, na kuendeleza usawa wa kijinsia kama kipaumbele cha kisiasa. 

Wamesema “Tunasikitishwa na kuongezeka kwa matumizi ya unyanyasaji wa kingono kama mbinu ya kikatili ya vita, mateso, ugaidi na ukandamizaji wa kisiasa, na tishio kwa usalama wa pamoja. Hatari ya kuwa mlengwa wa unyanyasaji wa kingono leo inazidishwa na ukweli kwamba uhalifu huu unaweza pia kuwezeshwa na kukuzwa mtandaoni, kwa kutumia chaneli za kidijitali.”

Badala ya kutumika vibaya wamekumbusha kuwa “Wakati huo huo, majukwaa ya kidijitali yanaweza kuwa na jukumu muhimu na kuwa chombo chenye nguvu cha kuboresha usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake na wasichana, na kuchangia katika kujenga uwezo wao wa kustahimili nyakati za shida. 

Wanaweza pia kusaidia katika kuzuia unyanyasaji wa kingono na kijinsia, na hatua zinazohitajika, kupitia tahadhari za  mapema na kuunganisha waathiriwa na njia za kuwatambulisha kwenye huduma, na kuwezesha kuripoti..”

Viongozi hao wameonya kwamba badala ya kuwa msaada kwa waathirika leo hii “Mitandao hiyo inatumika vibaya kusambala kauli za chuki na kuchochea ukatili wa kijinsia na ubaguzi, kwani kauli za chuki za kijinsia zinaendelea kuongezeka kutumika kuwanyamazisha watetezi wa haki za binadamu, na wanaharakati wa kisiasa kwa kuchagiza utekelezaji wa ukatili wa kingono. Katika mazingira yaliyoathiriwa na migogoro, majukwaa ya kidijitali yanatumiwa kusafirisha kiharamu wanawake na wasichana kwa madhumuni ya unyanyasaji wa kingono. Walanguzi wa ngono wanatumia mtandao kama zana ya kuajiri wanawake na haswa Watoto na kutangaza huduma za kinyonyaji.”

Wameongeza kuwa na katika mazingira mabaya zaidi wanawake na wasichana wanauzwa mtandaoni kama ilivypoainishwa kwenye maenmeo yanayodhibitiwa na kundi la kigaidi la ISIL

Zaidi ya hayo wamesema “ upotoshaji wa habari kwa makusudi na udhibiti kupitia kampeni za kutoa taarifa potofu unaathiri uwezo wa mataifa kulinda raia na kushughulikia unyanyasaji wa kingono. Matumizi ya intaneti kama silaha katika maeneo yenye migogoro pia huzuia waathiriwa wa unyanyasaji wa kingono unaohusiana na migogoro kupata taarifa kuhusu huduma za kuokoa maisha na kupata usaidizi wa mtandaoni kama vile usaidizi wa kisaikolojia.”

Kwa mantiki hiyo wametoa wito wa kuwa na “Majukwaa salama ya kidijitali yanayotii sheria za kimataifa, ili waathirika wa unyanyasaji wa kingono unaohusiana na migogoro na wale wanaowaunga mkono watumie mifumo hii kupambana na ukwepaji wa sheria na kudai uwajibikaji ulioboreshwa. Ni muhimu kukuza mazingira ya ulinzi mtandaoni na nje ya mtandao, ambayo yanazuia unyanyasaji wa kijinsia na vile vile kuwezesha kuripoti kwa usalama na makuchukuliwa hatua zinazofaa.”

Pia wameitaka Jumuiya ipambane kwa Pamoja dhidi ya tishio linaloongezeka kila mara linaloletwa na teknolojia ya kidijitali na kuziba pengo la mgawanyiko wa kidijitali wa kijinsia ili kuruhusu waathiriwa kupata rasilimali na kupambana na ukwepaji wa sheria kwa kuzingatia kujenga usawa wa kijinsia kwa kuzuia na kupambana na unyanyasaji wa kingono katika migogoro.

Wamehitimisha ujumbe wao kwa kusema kuwa “Kwa kushughulikia mgawanyiko wa kidijitali wa kijinsia, tunaweza kuunda ulimwengu ambapo wanawake na watoto wanaweza kuishi bila woga na vurugu.”

Siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili wa kingono katika mizozo huadhimishwa kila mwaka Juni 19 na mwaka huu imejikita katika kuhakikisha teknolojia inaunga mkono juhudi za kuzuia na kukomesha uhalifu huu, ikiwa ni pamoja na kuongeza fursa za ufikiaji huduma za intaneti na kuwawajibisha watu kwa matendo yao mtandaoni." 

Pakua

Audio Credit
Flora Nducha / Anold Kayanda
Audio Duration
3'11"
Photo Credit
UN