Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunapatia UNHCR dola milioni 3 kusaidia dharura ya elimu kwa wakimbizi wa Sudan: ECW

Tunapatia UNHCR dola milioni 3 kusaidia dharura ya elimu kwa wakimbizi wa Sudan: ECW

Pakua

Vita inayoendelea nchini Sudan mbali ya kukatili uhai wa mamia ya watu imesambaratisha na kupindua maisha ya mamilioni ya watu ikiwa ni pamoja na kuathiri huduma za msingi kama vile chakula, malazi, afya na elimu. Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa yanahaha kukidhi mahitaji ya dharura ya maelfu ya wakimbizi ndani na nje ya Sudan.

Asilimia kubwa ya waathirika ni wanawake na watoto ambao sasa mustakabali wao uko njia panda kwani elimu yao imekatizwa na vita hiyo. Kwa kutambua umuhimu wa elimu yao hata wakiwa ukimbizini mfuko wa kimatifa wa elimu haiwezi kusubiri ECW unashikamana na mashirika hayo kusaidia kunusuru elimu ya watoto hao kutoka Sudan. Juma hili ECW, imetangaza kuchagia dola milioni 3 kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR ili ziwasaidie watoto wakimbizi wa Sudan walioko nchini Chad kuweza kupata elimu ya dharura. Makala hii iliyoandaliwa na Flora Nducha inafafanua zaidi

Audio Credit
Assumpta Massoi/Flora Nducha
Audio Duration
5'22"
Photo Credit
ECW