Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tamu na chungu ya sarafu za kidijitali: UNCTAD yatoa mwongozo wa kisera

Tamu na chungu ya sarafu za kidijitali: UNCTAD yatoa mwongozo wa kisera

Pakua

Kamati ya  Umoja wa Mataifa wa Biashara na Maendeleo UNCTAD imetoa mapendekezo ya sera tatu zinazoweza kutumiwa na nchi zinazoendelea kufuatia kuongezeka kwa matumizi ya sarafu za kidijitali au Cryptocurrency wakati huu ambapo nchi nyingi hazina sera wala mifumo madhubuti ya udhibiti na matumizi yake kwa jamii. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi
 
Kamati hiyo ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD inasema, janga la COVID-19 lilivyoibuka duniani na watu kujitenga  ilikuwa vigumu kufanya biashara,  manunuzi na hata utumaji wa fedha kwa familia kutoka nchi moja kwenda nyingine na hivyo njia mbalimbali zilitumika hali iliyofanya hata nchi ambazo hapo awali hazitumii sarafu za kigijitali au Cryptocurrency kuanza kuzitumia.
Ingawa sarafu hizi ni za kibinafsi zimekuwa na manufaa na kuwezesha hata utumaji wa fedha, ni mali isiyo na utulivu na inaweza kuleta madhara kwa jamii na pia gharama kubwa.
Ni kwa mantiki hiyo hii leo UNCTAD imetoa miongozo mitatu ya kisera inayomulika hatari hizo: Mosi tisho la sarafu hizo kwenye utulivu wa kifedha, Pili: uhamasishaji wa rasilimali ndani ya nchi na tatu usalama wa mifumo ya kifedha.
Sera hizo tatu kwa pamoja zimeshauri nchi zinazoendelea masuala kadhaa ikiwemo, Kuhakikisha kuna udhibiti kamili wa kifedha wa sarafu zote za kidijitali na kupiga marufuku taasisi za kifedha zinazodhibitokushikilia sarafu pamoja na kushiriki katika biashara ya bidhaa zinazohusiana sarafu hizo.
Kuzuia matangazo yanayohusiana na sarafu hizo, kutoa mifumo ya malipo kwa umma iliyo salama, inayotegemewa na ya gharama nafuu inayoendana na ulimwengu tuliopo.
Mapendekezo mengine ni kukubaliana na dunia katika uratibu wa kodi na udhibiti na kushiriki katika utoaji wa taarifa na mwisho ni nchi hizo zinazoendelea kuhakikisha zinaweka udhibiti mpya wa mitaji ili kuzingatia vipengele vilivyowekwa na benki kuu za kila nchi, ambavyo havijawekwa na benki kuu na visivyojulikana kutokana na matumizi ya fedha hizi za kimtandao ambazo bado ni mfumo mpya kwa jamii nyingi.
TAGS : Crypocurrency, sarafu za kidigitali, Udhibiti, UNCTAD

Audio Credit
Assumpta Massoi/Leah Mushi
Audio Duration
2'8"
Photo Credit
Unsplash/André François McKenz