Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nafurahi sana ninapoona mjamzito kajifungua salama- Mkunga Erika

Nafurahi sana ninapoona mjamzito kajifungua salama- Mkunga Erika

Pakua

Umoja wa Mataifa hii leo umetoa ripoti yake kuhusu idadi ya watu ambapo idadi ya watu duniani inatarajiwa kuongezeka na kufikia bilioni 8 tarehe 15 mwezi Novemba mwaka huu wa 2022. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake wa siku hii anaweka bayana kuwa ongezeko hilo la idadi ya watu linatokana na sababu kadhaa ikiwemo maendeleo makubwa katika huduma za afya, maendeleo ambayo  yamechochea pia kupungua kwa vifo vya wajawazito na watoto wachanga. Huduma kwa wajawazito zimekuwa  bora na idadi ya wakunga inaongezeka kama huko Mexico ambako mkunga mwanafunzi anaona ndoto yake ya kuwa mkunga inatimia na tayari anachangia katika kupunguza vifo vya wajawazito na watoto kama anavyosimulia Thelma Mwadzaya katika makala hii iliyofanikishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na uzazi wa mpango, UNFPA.

Audio Credit
Anold Kayanda/Thelma Mwadzaya
Audio Duration
3'33"
Photo Credit
UNFPA Video