Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nashukuru Mungu, nashukuru Iran- Mkimbizi kutoka Afghanistan

Nashukuru Mungu, nashukuru Iran- Mkimbizi kutoka Afghanistan

Pakua

Iran, taifa hili la Mashariki ya Kati kwa miongo minne sasa limehifadhi zaidi ya wakimbizi 800,000 kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Afghanistan. Wakimbizi wanaowasili kando mwa shida za kusaka hifadhi ili waweze kuendeleza maisha  yao, kuna tatizo la afya.  Gharama za matibabu ni za juu na iwapo mkimbizi ana ulemavu hali inakuwa mbayá zaidi. Hali hiyo imemkumba Sultan Zoori mkimbizi kutoka Afghanistan aliyewasili Iran akiwa kwenye kitimwendo huku akihitaji huduma za afya zenye gharama ya juu. Awali hali ilikuwa si shwari lakini wahenga walinena, Mungu si Athumani, kulikoni? Ungana basi na Assumpta Massoi kwenye makala hii iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR.

Audio Duration
3'34"
Photo Credit
UNHCR Video