Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Michuano ya paralympic yaanza rasmi Tokyo Japan

Michuano ya paralympic yaanza rasmi Tokyo Japan

Pakua

Mashindano ya kimataifa ya Olimpiki ya watu wenye ulemavu yameanza rasmi hii leo mjini Tokyo Japani yakihusisha washiriki wa michezo mbalimbali kutoka kila pembe ya dunia wakiwemo wakimbizi. 

(TAATIFA YA FLORA NDUCHA) 
Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR mashindano hayo yanayojumuisha wanamichezo kutoka mataifa 160 kwenye michezo muhimu ya watu wenye ulemavu katika historia mwaka huu yana timu wa wakimbizi yenye washiriki sita wanaume watato na mwanamke mmoja wanaoshindana kwenye michezo mbalimbali ikiwemo kuogelea, kurusha tufe, mashindano ya boti na taekwondo. 

Huyo ni Parfait Hakizimana mkimbizi wa Burundi anayeishi kwenye kambi ya wakimbizi ya Mahama nchini Rwanda mmoja wa wanamichezo hao 6 wenye ulemavu wa timu ya wakimbizi akisema siku alipojua kuwa anashiriki mashindano ya Olmpiki Tokyo alifurahi sana na kuona milango imeanza kufunguka. 
Safari ya Parfait haikuwa rahisi amepitia zahma kubwa, machafuko na vita vilivyomwachia kilema cha maisha baada ya kupugwa risasi mwaka 1996 akiwa na umri wa miaka 6 tu na kupooza kabisa mkono wake wa kushoto, siku ambayo pia mama yake mzazi aliuawa.  

Lakini kama wasemavyo wahenga yaliyopita si ndwele bali kuganga yajayo Parfai anaganga yajayo kupitia michezo ambayo inampa nguvu, matumaini na ujasiri mkubwa. 

 “Michezo inatusaidia kuwa na ujasiri hata kama maisha ni magumu. Taekwondo ni maisha yangu, Napenda taekwondo kwani inanisaidia kusahau wakati mgumu nilioupitia katika maisha yangu.” 

Na kabla ya kuelekea Tokyo Parfait alipata fursa ya kuwaaga wanamichezo wenzake, kocha wake, ndugu jamaa na marafiki n ahata kupokea baraka toka kwa mkewe Irene 

“Kwangu ni furaha kubwa sana Mungu amzidishie na kumfungulia njia nzuri na ampatie nguvu ili afanikiwe tuje kusikia kuwa huko ameshinda” 

Kilichosalia sasa kwa Parfai ambaye pia amekuwa mwalimu wa taekwondo kwa wakimbizi wengine kambini Mahama ni kupeperusha vyema Tokyo bendera ya wakimbizi  na kutimiza ndoto yake huku akitakiwa kila la heri na kushangiliwa na watu milioni 82 waliotawanywa kote duniani wakiwemo milioni 12 kati yao wanaoishi la ulemavu. 
 

Audio Credit
Grace Kaneiya /Flora Nducha
Audio Duration
2'19"
Photo Credit
UNPA