Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtoto wa kiume atumbia mbinu kuepusha mtoto wa kike kuozwa

Mtoto wa kiume atumbia mbinu kuepusha mtoto wa kike kuozwa

Pakua

Nchini Ethiopia ambako asilimia 40 ya wasichana wanaolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18, msichana Tsigist Wudu Chekol ilikuwa kidogo tu awe miongoni mwa hao lakini akaponea chupuchupu na sasa ni mwanachama wa kikundi cha wasichana katika shule anayosoma, kinachopambana kuhakikisha katika jamii hakuna mtoto anayeolewa kabla ya wakati. Ahimidiwe Olotu na maelezo zaidi.

Ni asubuhi, katika jamii zilizoko pembezoni chini Ethiopia. Mtoto wa kiume ambaye amejiandaa tayari kwenda shuleni, anaandika maelezo kwenye kipande cha karatasi. Amesikia kuhusu mipango ya ndoa ambayo inamuhusu mtoto mwenzake  anayeitwa Zemenay. 

Kipande hiki cha karatasi anakitumbukiza katika kasha dogo ambalo limetundikwa katika ukuta wa moja ya majengo ya shule. Baadaye mwalimu anayesimamia kikundi cha wasichana wanaopambana na ndoa za utotoni, atakichukua na kusoma taarifa hiyo ili hatua ichukuliwe. 

Huyu ni Tsigist Wudu Chekol mwenye umri wa miaka 16, mwanachama wa kikundi hicho cha wasichana ambaye kama si msimamo wake wa kutaka kuendelea na masomo, angeozwa na wazazi wake alipokuwa na umri wa miaka 13. 

Haikuwa kazi rahisi kuyabadili mawazo ya wazazi, kwani wao wanaamini maisha yake yangekuwa bora kama angeolewa. Lakini hakukata tamaa na kwa kushirikiana na shule yake, wakafanikiwa kuizuia ndoa hii. 

Tsigist anashiriki vikao kikundi cha wasichana shuleni. Kikao kama hiki cha kujadili taarifa iliyoletwa kuhusu ndoa inayopangwa dhidi ya mtoto Zemenay. Zemenay mwenyewe hata hakuwa na taarifa kuwa wazazi wanapanga aolewe, kwa hivyo wasichana wenzake hawa wameongea naye, na taarifa imepelekwa kwenye  muungano wa wanaopinga ndoa za utotoni katika jamii na hivyo kuitishwa kikao cha wanajamii. 

Wiki mbili baada ya kikao, wazazi wa Zemenay, wanakubali kuisitisha ndo hiyo. 

Audio Credit
Flora Nducha/Ahimidiwe Olotu
Audio Duration
1'48"
Photo Credit
UNICEF/ Ethiopia/2018/Mersha