Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kijana, lazima utunze vizuri kumbukumbu za biashara yako ili uaminike-Ashford Kariuki

Kijana, lazima utunze vizuri kumbukumbu za biashara yako ili uaminike-Ashford Kariuki

Pakua

Ashford Kariuki ni kati ya vijana ambao wamenufaika na mkopo kutoka kwa hazina ya maendeleo ya vijana nchini Kenya ambayo ilibuniwa kwa lengo la kuwainua vijana walio na ndoto za kujiajiri na kujiendeleza kimaisha. Baada ya masomo ya shule ya upili alianzisha biashara ya kuwauzia wakulima chakula cha mifugo. Mwaka uliopita alifanikiwa kupata mkopo wa lori kutoka hazina hiyo ya vijana ikiwa ni hatua kubwa katika biashara yake. Amezungumza na mwandishi wetu wa nchini Kenya, Jason Nyakundi.

Audio Credit
Grace Kaneiya/ Jason Nyakundi
Audio Duration
3'35"
Photo Credit
©FAO/Natalia Merkusheva