Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu bilioni 1 duniani wanaishi na matatizo ya akili-Takwimu

Watu bilioni 1 duniani wanaishi na matatizo ya akili-Takwimu

Pakua

Kuelekea siku ya afya ya akili duniani itakayoadhimishwa kesho Jumamosi Oktoba 10, takwimu zinaonesha kuwa takribani watu bilioni 1 duniani kote wanaishi na matatizo ya akili. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake kwa siku hii amesema, inabidi hatua zichukuliwe ili kuhakikisha kunakuwa na huduma bora ya afya ya akili kwa wote kwani hivi sasa inaonesha pia kuwa kila sekunde 30 mtu mmoja anajiua kutokana na tatizo hili la afya ya akili. 
Siku ya afya ya akili duniani ya mwaka huu wa 2020 inaadhimishwa wakati maisha ya watu wengi yamechukua mkondo tofauti kutokana na mlipuko wa virusi vya corona. Miezi kadhaa  iliyopita kumeshuhudiwa changamoto za kila aina zikiwemo watu kupoteza ajira, kuishi kwa hofu na hata kufariki kwa watu. Lakini pia kuna matatizo ya akili ambayo huwakumba watu tangu wanapozaliwa hadi wanapokua watu wazima.
Jason Nyakundi ameandaa makala ifuatayo akianza kuzungumza na mzazi aliye na mtoto mwenye changamoto ya akili.

 

Audio Credit
Flora Nducha- Jason Nyakundi
Sauti
5'42"
Photo Credit
WHO/P. Virot