24 JULAI 2020

24 Julai 2020

Katika jarida la mada kwa kina hii leo kutoka Umoja wa Mataifa  Flora Nducha anakuletea

-Balozi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Kenedy Gastorn amesema kifo cha aliyekuwa rais mstaafu wa Tanzania Benjamin William Mkapa si pigo kwa Tanzania tu bali kwa Afrika na Jumuiya ya kimataifa kutokana na mchango wake mkubwa katika masuala ya amani

-Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa leo imesema inatiwa wasiwasi na taarifa kwamba serikali ya Zimbabwe huenda inatumia janga la COVID-19 kama chambo cha kubinya uhuru wa kukusanyika na kujumuika

-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR  limetoa wito kwa mataifa kuwaachilia wakimbizi na waomba hifadhi walio mahabusu kinyume cha sheria na kuwalinda na janga la COVID-19

-Mada yetu kwa kina leo inamlenga msanii mashuhuri wa uchoraji na uchongaji kutoka Tanzania 

-Na katika kujifunza Kiswahili utasikia maana za neno "TRELA" kutoka kwa mchambuzi wetu Onni Sigalla wa BAKITA Tanzania

Audio Credit:
UN News/Flora Nducha
Audio Duration:
10'44"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud