Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Walinda amani wanawake kutoka Tanzania wasema, "wanawake DRC wanafunguka zaidi kwetu kuelezea masahibu yao."

Walinda amani wanawake kutoka Tanzania wasema, "wanawake DRC wanafunguka zaidi kwetu kuelezea masahibu yao."

Pakua

Kuelekea siku ya walinda amani duniani kesho Mei 29, siku ambayo mwaka huu inamulika wanawake walinda amani wa Umoja wa Mataifa na mchango wao katika ujenzi wa amani ya kudumu, tunamulika askari wanawake wa Tanzania. Wanawake hao walinda amani wanahudumu katika kikundi cha saba cha Tanzania, TANZBATT 7, cha kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO kama anavyosimulia Assumpta Massoi .

Kwenye kata ya Matembo mjini Beni katika jimbo la Kivu Kaskazini, nchini DR Congo, shamrashamra za mapokezi ya vifaa vya shule kutoka kwa wanajeshi wanawake watanzania walioko TANZBATT 7 huko Beni.

Uwepo wa wanawake kwenye ulinzi wa amani ni kufuatia azimio namba 1325 la mwaka 2000 lililoona umuhimu wa kujumuisha kundi hili ili amani iwe ya kudumu na endelevu.

Wanawake hawa walinda amani wanatoa huduma mbalimbali ambapo mmoja wao, Private Diana Mushi anasema kwa kufanya kazi hii amejifunza madhara ya vita kwa wanawake, wajawazito, watoto na wazee na zaidi ya hapo,

“Tunakuwa tunawatembelea mara kwa mara na kusaidiana nao kimawazo, na kuelekezana katika ujasiriamali, na pia kutoa elimu kwa wazazi jinsi ya kuwalea watoto, na pia kuwaelimisha wanafunzi ili wasikate tamaa kulingana na hali iliyopo DRC”

Private Diana akaangazia pia umuhimu wa askari wa kike kwenye ulinzi wa amani akisema

“Wanawake wa DRC wanaathirika na mambo mengi ambayo mengine wanashindwa kuzungumza na wanaume, inapaswa kuongea na wanawake wenzao tukiwemo sisi askari wa kike, na tumekuwa tunazungumza nao wanatuambia shida zao nyingi na sisi tunapeleka ujumbe ngazi za juu na kuweza kusaidiwa kulingana na matatizo yao.”

Azimio namba 1325 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitishwa tarehe 31 mwezi Oktoba mwaka

Audio Credit
Flora Nducha/Assumpta Massoi
Audio Duration
2'13"
Photo Credit
TANZABATT 7/Ibrahim Mayambua