Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COVID-19 kusababisha mamilioni ya watoto kukosa mlo shuleni

COVID-19 kusababisha mamilioni ya watoto kukosa mlo shuleni

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limesema takribani Watoto milioni 300 sasa wanakosa huduma yam lo shuleni kutokana na virisi vya corona, COVID-19 vilivisababisha maelfu ya shule kufungwa kote duniani. Flora Nducha na taarifa zaidi

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

Shirika hilo linasema lina jukumu kubwa la kuhakikisha msaada wa chakula kwa watu milionin 87 kote duniani huku likisaidia juhudi za kukabiliana na mlipuko wa COVID-19.

Hivi sasa zaidi ya vijana na Watoto milioni 860 karibu nusu ya wanafunzi wote duniani wamelazimika kukaa nyumbani mbali na shule na vyuo vikuu kwa sababu ya COVID-19. Nchi zaidi ya 100 zimefunga shule zake zote nchi nzima na zingine zinaendelea kufuata nyayo. Akizungumxza na waandishi wa habari mjini Geneva hii leo msemahi wa WFP Elisabeth Byrs amesema 

(SAUTI YA ELISABETH BYRS)

"Kwa sababu ya mlipuko wa COVID Watoto milioni 300 wa shule za msingi wanakosa mlo mashuleni ambao wanautegemea . Takribani nchi 30 ambako WFP inaendesha programu ya mlo shuleni kumeripotiwa shule kufungwa nchi zima au kwa sehemu kubwa  na hii inamaanisha kwamba takribani watoto milioni 9 hawapati tena mlo shuleni unaotolewa na WFP na kwamba idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka katika siku na wiki zijazo."

Hivi sasa WFP inashirikiana na wadau na washirika wake kuhakikisha kwamba wanafunzi na familia zao wanaendelea kupokea msaada ambao unashughulikia mahitaji yao ya chakula na lishe wakati huu wa mgogoro wa COVID-19.

Na kwa shule ambazo bazo hazijafungwa WFP inasema kipaumbele ni kuhakikisha usafi na kuzingatia viwango vya usalama wa chakula vinafuatwa ili kupunguza hatari ya maambukizi.

Shirika hilo linasema kwa nchi ambako shule zimefungwa linafanya tathimini ya uwezekano wa njia mbadala ya kuwasaidia watoto. Njia hizo ni pamoja na kutoa mgao wa chakula wa kwenda nao nyumbani, kuwafikishia chakula nyumbani na kutoa fedha taslim au vocha.

Pia kwa nchi ambako program za dharura zimeanzishwa na serikali WFP inapigia chepuo ujumuishwaji wa watoto wa shule za msingi katika program hizo.

Mpango wa WFP wa mlo mashuleni unaendeshwa katika nchi 61 duniani na unatumika kama ngao muhimu ya ulinzi  wa kijamii hasa kwa Watoto masikini na familia zisizojiweza.

Audio Credit
Arnold Kayanda/Flora Nducha
Audio Duration
2'25"
Photo Credit
WFP/Alexis Masciarelli