Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN Environment na harakati za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

UN Environment na harakati za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

Pakua

Suala la mabadiliko ya tabianchi ni changamoto ambayo nchi zinakabiliana nazo kote ulimwenguni. Umoja wa Mataifa kupitia mashirika uko mstari wa mbele sio tu kuchagiza kuhusu ulinzi wa mazingira lakini pia kushirikiana na nchi kukabiliana na athari hizo. Akiwa Tanzania wiki hii kushiriki mkutano wa kujadili mwelekeo wa mkutano wa mwezi ujao jijini New York Marekani wa hatua dhidi ya Tabianchi, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa UN Environment, Joyce Msuya alizungumza na waandishi wa habari ambapo ametaja baadhi ya kazi wanazozifanya kuimarisha mazingira lakini pia kutolea mifano ya hatua zilizopigwa hususan barani Afrika. Kwanza anaanza na upana wa suala la mabadiliko ya tabianchi

Audio Credit
Grace Kaneiya/ Joyce Msuya
Audio Duration
5'15"
Photo Credit
Laurean Kiiza/UNIC Dar es salaam