Kuna changamoto katika ufikiaji elimu ya awali Tanzania-UNICEF Tanzania

8 Agosti 2019

Elimu ya awali ni nguzo muhimu katika kujengea mtoto uwezo wa kusoma na kuhesabu hata baadaye ikilinganishwa na watoto ambao hawakupata elimu hiyo.

Mapema mwaka huu shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema elimu ya awali ni msingi muhimu ambapo elimu ya baadaye inategemea kwa kiasi kikubwa mafanikio ya elimu hiyo. Hata hivyo watoto wengi duniani kote wanakosa fursa hiyo muhimu na hivyo kuongeza hatari ya kurudia madarasa au hata kutoendelea na masomo na hivyo kuwatenganisha na wanafunzi wenzao ambao wao walihudhuria.

Katika kutaka kufahamu hali ya ushiriki wa watoto katika elimu ya awali nchini Tanzania, Stellla Vuzo wa kituo cha habari za Umoja wa Mataifa, UNIC jijini Dar es Salaam nchini Tanzania amezungumza na Audast Muhinda, afisa kitengo cha elimu katika UNICEF ambapo Bwana  Muhinda katika sehemu hii ya kwanza ya makala anaanza kwa kuangazia ripoti hiyo

Audio Credit:
Arnold Kayanda/ Stella Vuzo
Audio Duration:
3'47"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud