Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chumia juani ujanani ili ulie kivulini uzeeni (Sehemu ya pili)

Chumia juani ujanani ili ulie kivulini uzeeni (Sehemu ya pili)

Pakua

Ule usemi wa wahenga ya kwamba mchumia juani  hulia kivulini ni suala ambalo linaonekana kuwa na mashiko iwapo litapatiwa mtazamo mpana zaidi na kuhusishwa na maisha ya sasa na baadaye. Hoja hii pamoja na kumaanisha wakati mwingine kuwa fanya kazi kwa bidii ili ule matunda yake ukiwa umetulia, nchiniUganda imechukuliwa pia  kwamba ni vyema mtu akiwa kijana aweke akiba yake ili anapokuwa mtu mzima au mzee aweze kuishi maisha yaliyo bora zaidi.

Hatua hiyo ni muhimu kwa kuzingatia pia wakati mwingine malipo ya uzeeni ambayo yanatambuliwa hata na Umoja wa Mataifa kuwa ni haki ya msingi ya kila mkazi bado husuasua na hayakidhi mahitaji.

Katika Sehemu hii ya pili ya makala yetu  John Kibego, mwandishi wetu kutoka Uganda ameendelea kuzungumza na  Mzee Ashrafu Nyorano Mugeny akiwa nyumbani kwake Butanjwa, kiunga cha mji wa Hoima wakitathimini ukweli kwamba“kioo cha maisha yako ya ujana ni maisha uzeeni”, yaani unapochezea maisha ni kero uzeeni. Ungana nao katika sehemu hii ya kwanza

Audio Duration
4'3"
Photo Credit
UNDP Uganda/Luke McPake